Hunywi maji yakapita Me nkiguna ushafika Jina gani hujaniita baby Ushauri hutaki kabisa Eti uniache nna visa Vya vifarauni na musa vingi Nikilala naota kama unaniita Nafumba macho navuta shuka Naona napumbazika Unishikapo ndipo hapo nafarijika Mambo yako mahaba yako Ndo maana natononoka we
Wana wana wana wana Pale tulipokutana Mikono tukapeana Macho yakatizamana Wana wana wana wana Pale tulipokutana Namba kubadilishana Nafsi kukubaliana aah!
Nzi kidonda nimefia Wahenga walisema Maradhi yaweza yasiwe na dawa Kwa penzi yakapona Rabii amenipa nusura Jeuri sina tena We ndo ganzi umenimaliza hasira Siumwi wakisema Nidekeze niliwaze Washushuke wanyamaze Nikuna nibembeleze Usinipepee nipulize Watuone washituke Roho zao ziwaume Mi nipike ule chote Unenepe upendeze
Wana wana wana wana Pale tulipokutana Mikono tukapeana Macho yakatizamana Wana wana wana wana Pale tulipokutana Namba kubadilishana Nafsi kukubaliana aah!
Ukitaka uniweze nibebe wewe Ukipenda unibimbe unikumbatie Hata watu watuone wakahadithie Nitambulishe niringe niwavimbie Ukitaka uniweze nibebe wewe Ukipenda unibimbe unikumbatie Hata lizer atuone akahadithie Nitambulishe nitambe niwavimbie